Kitaifa
-
Dar-es-salaam | Kikao cha kufunga mwaka wa 2025 cha Jamiat Al-Mustafa International Foundation baina ya Wanafunzi na Mkuu wa Chuo
Washiriki walipata nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo ya kuboresha utendaji wa Taasisi. Mazungumzo yalikuwa ya kujenga baina ya Mkuu wa Chuo na Wanafunzi, na yalilenga kuweka mikakati madhubuti kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo unaofuata.
-
Burkina Faso: Daktari Aliyemkosoa Rais Traoré Atumwa Vitani kupambana na Magaidi Baada ya kupata Mafunzo ya Kijeshi - Kisa Kinachozua Mjadala Mpana
Rais Ibrahim Traoré, akizungumza katika mahojiano ya televisheni ya kitaifa, alithibitisha tukio hilo na kusema kwa maneno makali: “Kama kuna daktari, mwalimu, au mfanyabiashara anayehisi anajua zaidi kuhusu vita kuliko wanajeshi wetu, basi ni bora naye achangie kwa vitendo - aende vitani.”
-
Katika Kujibu Ukosoaji Kuhusu Nafasi ya Misri katika Mgogoro wa Gaza, Rais Abdel Fattah al-Sisi: “Tunajilinda Tu!”
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amejibu ukosoaji wa kimataifa kuhusu nafasi ya nchi yake katika mgogoro unaoendelea wa Gaza, akisisitiza kuwa jukumu lake kuu ni kulinda usalama na afya ya watu wa Misri, na kwamba nchi yake “inajilinda tu.”
-
Maulid Adhimu ya Mtume (s.a.w.w) Temeke Mwisho - Dar-es-salaam kuvutia wageni wa kitaifa na Kimataifa - Maandalizi yakamilika kwa Kiwango cha Juu
Dr. Alhad Mussa Salum ametoa wito kwa Waumini kuhudhuria kwa wingi, akisisitiza umuhimu wa kumuadhimisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa upendo na amani.
-
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania:
Viongozi wa Kitaifa wa JMAT-TAIFA Wajadili Ajenda za Amani na Maridhiano Jijini Arusha
Askofu Profesa Rejoice Ndalima: "Inafaa na inapendeza kwa viongozi wa kijamii na kidini kuungana ili kupunguza migawanyiko na kuondoa maneno ya chuki miongoni mwa Wananchi".
-
Kurefushwa kwa Muda wa Kutuma Kazi za Mkutano wa Kitaifa wa Swala hadi Septemba 31
Mwenyekiti wa Kamati ya Kisayansi ya Mkutano wa Kitaifa wa Kusimamisha Swala ametangaza kuwa muda wa kutuma kazi za utafiti na maandiko kwa ajili ya mkutano huo umeongezwa hadi tarehe 31 Septemba, kutokana na mwitikio mkubwa wa watafiti na washiriki.