Muhammad(s.a.w.w)

  • Ushahidi wa Mawalii Katika Kumfananisha Ali na Manabii

    Ushahidi wa Mawalii Katika Kumfananisha Ali na Manabii

    Ali (a.s), wapo Watu waliodai kuwa wanampenda, mpaka wakamfanya kuwa ni mungu, ametakasika Mwenyezi Mungu na wanayo mshirikisha nayo. Na wapo watu waliomchukia na wakampiga vita, wakamtukana na kumlaani, wakakufuru na wakatoka katika Uislamu. Na wapo baadhi ya Watu waliompenda, wakawa watiifu kwake, na wakashikamana naye kama alivyoamrisha Mtume (s.a.w.w), basi kwa hakika hao ndio waumini wa kweli.