Ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s.) ni shule kamili ya roho, akili, jamii, na siasa. Ni fursa ya kuimarisha imani, kukuza undugu, kupandikiza roho ya kupinga dhulma, na kudumisha kumbukumbu ya kujitolea kwa ajili ya haki. Kuendeleza ibada hii ni njia ya kudumisha maadili ya kimungu na kibinadamu, na kuisambaza kwa vizazi vijavyo.
Safari ya Arubaini katika Ardhi ya Karbala, inatengeneza Ukaribu wa Kiroho na Hussein (a.s) Katika Kila Hatua unayoipiga ukielekea kumzuru Aba Abdillah Al-Hussein (as).