Vikosi vya usalama vya Iran vimemkamata mtu anayedaiwa kuwa wakala wa Mossad wakati wa maandamano yanayoendelea, kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa ujasusi kupitia Instagram. Mamlaka zinasema mtuhumiwa ana uhusiano na shirika lenye makao yake Ujerumani, huku uchunguzi ukiendelea kubaini ukubwa wa shughuli zake.
Kwa mujibu wa madai ya tovuti moja ya Kizayuni, vyanzo vya kisiasa nchini Israel vinamtaja David Barna, mkuu wa Mossad, kama mmoja wa wagombea wakuu wa kumrithi Benjamin Netanyahu.
Maafisa wa Lebanon wameripoti kwamba angalau watu 32 wamekamatwa kwa tuhuma za kushirikiana na Mossad na kupeleka taarifa za kina kuhusu nafasi na harakati za Hezbollah kwenda Israel wakati wa vita vya hivi karibuni.