15 Desemba 2025 - 15:05
Matokeo ya Miaka Miwili ya Mauaji ya Kimbari Dhidi ya Wanawake na Watoto Gaza na Uwezekano wa Kujijeruhi kwa Wazayuni!

Gazeti la Sydney Morning Herald lilithibitisha kuwa katika tukio hili watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa, huku idadi kubwa ya washiriki wa sherehe hizo wakikimbilia maeneo tofauti na kujificha.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- leo vyanzo vya Australia vimeripoti kutokea kwa tukio la ufyatulianaji wa risasi kwa kiwango kikubwa wakati wa sherehe za Hanukkah katika eneo la Bondi Beach, jijini Sydney.

Kabla ya kulichambua tukio hili kwa mtazamo wa magazeti na vyombo vya habari vya Australia na vya Kizayuni, inaonekana kuna swali muhimu sana: Kwa nini sherehe za Kiyahudi zinazohusishwa na uungaji mkono wa Uzayuni zinakuwa shabaha ya mashambulizi?! Ukweli ni kwamba, matokeo ya makumi ya uhalifu na mauaji yanayofanywa na utawala wa Israel nchini Palestina, pamoja na miaka miwili ya mashambulizi yasiyokoma dhidi ya Gaza, si chochote ila kuifanya dunia nzima isiwe salama kwa vipengele vya Kizayuni.

Ni lazima kukiri kuwa, siku baada ya siku hali itazidi kuwa ngumu kwa utawala wa Kizayuni.

Gazeti la Sydney Morning Herald lilithibitisha kuwa katika tukio hili watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa, huku idadi kubwa ya washiriki wa sherehe hizo wakikimbilia maeneo tofauti na kujificha.

Polisi wa Australia walitangaza kuwa “operesheni ya kiusalama inaendelea katika eneo la Bondi Beach,” na wakatoa wito kwa raia kuepuka eneo hilo. Pia walibainisha kuwa watu wawili wamekamatwa kufuatia taarifa za ufyatulianaji wa risasi.

Kwa upande mwingine, Isaac Herzog, rais wa utawala wa Kizayuni, aliitaka serikali ya Australia kushughulikia kile alichokiita “wimbi kubwa la chuki dhidi ya Wayahudi linalolenga jamii za Kiyahudi nchini humo.”

Gazeti la Kizayuni Yedioth Ahronoth liliripoti kuwa ufuo wa Bondi ulikuwa mwenyeji wa sherehe za sikukuu ya Kiyahudi ya Hanukkah, na kubainisha kuwa takribani watu 2,000 walihudhuria sherehe hiyo iliyolengwa.

Baada ya tukio hili, maafisa wa Kizayuni wameanza kutoa tuhuma; hata hivyo, mitazamo tofauti inaendelea kusambazwa ikieleza kuwa huenda shambulio dhidi ya Wayahudi wa Sydney lilipangwa na Israel yenyewe. Sababu ni kwamba Wazayuni na utawala wa Israel wamepoteza nafasi na hadhi yao ya kimataifa kutokana na uhalifu wa miaka miwili ya hivi karibuni huko Gaza na Lebanon, na kwa ajili ya kuirejesha hadhi hiyo, hawana njia nyingine isipokuwa kujionesha kama waathirika.

Katika tukio la tarehe 7 Oktoba pia, kulikuwepo ushahidi wa aina hii ya kujionesha kama waathirika kwa upande wa Wazayuni, kiasi kwamba wako tayari hata kuwatoa kafara watu wao wenyewe kwa lengo hilo. Katika operesheni ya 7 Oktoba, helikopta za Israel ziliwaua mamia ya Wazayuni.

Baada ya utawala wa Israel kunufaika kisiasa na tukio hilo na baada ya kusambazwa kwa picha, jambo hilo awali lilikataliwa; lakini baadaye wakadai kuwa kilitokea “kwa makosa”!

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha