Lengo la tukio la kusoma Dua kila siku ya Alhamisi, ni: Kuimarisha maadili ya kiroho miongoni mwa wanafunzi. Kuendeleza mazoea ya kusoma dua za Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s). Na kufanya upya ahadi na mapenzi yetu kwa Imam Mahdi (a.t.f.s).
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ufuatao ni Ufafanuzi wa Tukio la Dua ya Siku ya Alhamisi:
Katika tukio hili la kiroho, dua maalum ya siku ya Alhamisi inasomwa kwa pamoja na wanafunzi wa shule. Baada ya kumalizika kwa usomaji wa dua hiyo, Dua ya Faraj (dua ya kumuomba Mwenyezi Mungu alete faraja kwa kumdhirisha kwa haraka Imam Mahdi – (a.t.f.s) inasomwa kwa pamoja kwa sauti moja na wanafunzi wote.
Lengo la tukio hili ni:
Kuimarisha maadili ya kiroho miongoni mwa wanafunzi.
Kuendeleza mazoea ya kusoma dua za Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s).
Kufanya upya ahadi na mapenzi kwa Imam Mahdi (a.t.f.s).
Wakati wa Tukio ni: Kila siku ya Alhamisi.
Mahali: Ukumbi wa Swala wa Hawza ya Imam Zayn al-‘Ābidīn (a.s).
Your Comment