Jenga Mustakbali wa Mtoto Wako kwa Elimu Bora, Ujuzi wa Teknolojia na Ajira Bora – Fursa Hii Usiiache!


Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Chuo cha Al-Mustafa – International Foundation – Dar-es-Salaam, Tanzania kinakutangazieni Nafasi za Masomo kwa mwaka mpya wa masomo wa 2026 - kama Ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Waheshimiwa Wazazi;
Uongozi wa Chuo cha Al-Mustafa – International Foundation – Dar-es-Salaam – Tanzania unatumia fursa hii kukufahamisheni juu ya uwepo wa fursa adhimu katika chuo hiki kwa ajili ya mustakbali mwema wa watoto wenu.

Kando na kupata Elimu ya Dini Tukufu ya Kiislamu, watoto wenu wapendwa wanaweza pia kupata elimu na ujuzi katika kozi mbalimbali zenye umuhimu mkubwa kwa ajili ya kumuwezesha na kumuongezea mwanafunzi uwezo wa:
✅ Kupata ajira kwa haraka baada ya chuo.
✅ Kujiajiri kwa kutumia ujuzi wa teknolojia.
✅ Kuendana na mabadiliko ya kidijitali duniani.
✅ Kuelekea kwenye taaluma zenye malipo mazuri.

Chuo kinatoa Kozi Zifuatazo:
1_Ushonaji na Ufundi Chereheni (kwa Wanafunzi wa Kike)
2_Kozi ya Umeme - Uhandisi wa Umeme na Ufungaji Umeme (kwa Wanafunzi wa Kiume).
3_Kozi mbalimbali za Kompyuta
4_Lugha ya Kiingereza.
5_Lugha ya Kiarabu.
6_Kozi ya Kilimo.

7_QT (Qualifying Test) – Mafunzo ya Kidato cha Nne kwa wale waliokosa nafasi ya shule za kawaida
8_Form Four Resitters – Kurudia Mtihani wa Kidato cha Nne.

Kuhusu Chuo:
Chuo cha Jamiat Al-Mustafa (s) – Dar-es-Salaam, Tanzania ni chuo bora kabisa nchini Tanzania chenye usajili kamili kwa ajili ya kuendelea na harakati zake za utoaji wa maarifa katika:

1_Sayansi za Kiislamu (Islamic Sciences)
2_Na Sayansi za Kibinadamu (Humanities).
Kupitia kibali na usajili wake kamili, Uongozi wa Chuo umeazimia na kukusudia kukuletea fursa hizi muhimu kwa ajili ya watoto wenu Wapendwa, ambazo zitaanza kwa mwaka mpya wa masomo wa 2026.

Vyuo Vyetu Vinapatikana:
Mbezi Beach – Dar-es-Salaam (Chuo cha Wavulana).
Kigamboni – Dar-es-Salaam (Chuo cha Mabinti).

Tanbihi:
1_Chuo cha Mabinti Kigamboni - Masomo yake yote yanaendeshwa kwa Lugha ya Kiingereza.
2_Mwanafunzi atakayepokelewa katika Chuo hiki ni yule aliyemaliza Form Four (Mwenye Cheti cha Form Four).
3_Mwanafunzi atafundishwa Lugha ya Kiingereza kwa muda wa mwaka mmoja ili kuimarishwa katika uzungumzaji na uelewa wa Lugha ya Kiingereza kwa kuzingatia kuwa Kiingereza ndio Lugha rasmi inayotumika katika Masomo yake yote katika Chuo hiki.

Jenga Mustakbali Mzuri wa Mtoto Wako kwa Elimu Bora Ujuzi wa Teknolojia na Ajira Bora Kupitia Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam - Tanzania, Fursa Hii Usiiache!

Wasiliana Nasi:
+255 745 993 522 | +255 745 002 259 | +255 781 119 113

Wahi Kujisali - Nafasi ni Chache
Tafadhali Bonyeza Klipu hiyo hapo chini kusikiliza Tangazo Hili
Your Comment