Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na kiserikali, likiongozwa na Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- DAR ES SALAAM, 27 Oktoba 2025 - Kongamano kubwa la Amani ya Kitaifa limefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), likilenga kujadili na kuhimiza umuhimu wa kudumisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025.
Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na kiserikali, likiongozwa na Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji).

Miongoni mwa viongozi wa kidini waliohudhuria ni Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, ambaye alisisitiza umuhimu wa kuendeleza mazungumzo ya amani, umoja wa kitaifa, na mshikamano miongoni mwa Watanzania wote bila kujali tofauti za kidini au kisiasa.
Washiriki wa kongamano hilo walikubaliana kuwa amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo, wakitoa wito kwa wananchi kushiriki katika zoezi la upigaji kura kwa utulivu, umoja na heshima kwa sheria za nchi.

Kaulimbiu ya kongamano hilo ilikuwa:
“Kupiga Kura ni Haki Yetu, Kulinda Amani ni Wajibu Wetu.”
Kongamano hilo limeacha ujumbe muhimu wa kuimarisha mshikamano wa kitaifa na kuonyesha mfano bora wa ushirikiano kati ya viongozi wa dini na serikali katika kulinda amani ya Tanzania.

Your Comment