Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Abna lenye kunukuu kutoka RT, "Ro Khanna", mwanachama wa Congress ya Marekani kutoka chama cha Democratic, alitaka kamati ya kitaifa ya Wanademokrasia (DNC) ichapishe ripoti ya uchambuzi wa uchaguzi wa 2024.
Alisema: Kushindwa kwetu kukomesha mauaji ya kimbari huko Gaza kulitugharimu kupoteza uungaji mkono.
Ufichuzi unaonyesha kuwa uungaji mkono wa utawala wa Kizayuni huko Gaza umesababisha wapiga kura vijana, vikosi vya kimaendeleo na Wamarekani wenye asili ya Kiarabu na Waislamu kujiondoa kutoka kwa chama cha Democratic nchini Marekani katika uchaguzi wa 2024.
Utawala wa Kizayuni, kwa kimya cha jumuiya ya kimataifa na kwa kuliungwa mkono na Marekani, hadi sasa umeua zaidi ya raia 70,000 huko Gaza wakiwemo wanawake na watoto.
Your Comment