-
Afisa wa nne wa Wizara ya Mambo ya Nje ya US ajiuzulu kupinga sera kuhusiana na vita vya Ghaza
Msemaji wa kitengo cha Kiarabu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amejiuzulu wadhifa wake kulalamikia na kupinga sera za serikali ya nchi hiyo katika vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
Jamaica yatambua rasmi taifa la Palestina
Jamaica inasema imeamua kuitambua rasmi Palestina kama taifa huku kukiwa na wasiwasi wa muda mrefu juu ya vita vya Israel vinavyoendelea katika Ukanda wa Gaza na mzozo mbaya wa binadamu katika eneo hilo lililozingirwa.
-
Spika wa zamani wa Marekani: Netanyahu anapaswa ajiuzulu, amekwamisha amani kwa miaka kadhaa
Spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi amesema, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ni kizuizi cha kupatikana amani Ghaza na anapaswa ajiuzulu.
-
Tume ya Haki za Binadamu ya Ulaya: Uingereza isitishe mpango wa kuwapeleka wahamiaji huko Rwanda
Tume ya Kutetea Haki za Binadamu ya Ulaya, imetoa wito kwa Uingereza kutupilia mbali mpango wake wenye utata wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda.
-
Hamu ya Wamarekani kupiga kura imepungua kwa kiwango kisicho na mfano
Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na Chaneli ya NBC News umeonyesha kuwa, Wamarekani wanapoteza hamu ya kupiga kura katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu kwa sababu mgombea wa chama cha Democrat Joe Biden na mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump, wote wawili hawana mvuto kwa wapiga kura.
-
"Biden atakuwa msaliti kama atasaini msaada mpya kwa utawala wa Kizayuni"
Jumuiya ya Waislamu wa Marekani imetangaza kuwa, rais wa nchi hhiyo Joe Biden atakuwa msaliti kama atasaini msaada mpya wa kijeshi kwa utawala wa Kizayuni unaoua kwa umati watoto wadogo huko Ghaza na atakuwa amevuruga kabisa uhusiano wake na Waislamu.
-
Msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola bilioni 26 wa Marekani kwa Israel sambamba na vita vya Gaza
Baada ya mabishano na mvutano kati ya Wademokrat na Warepublican na Hitilafu za pande hizo mbili juu ya msaada wa kigeni, Baraza la Wawakilishi la Marekani limeidhinisha kifurushi cha msaada wa dola bilioni 60 kwa Ukraine na kifurushi kiingine cha dola bilioni 26 kama msaada wa kijeshi kwa Israel kwa kura 366 dhidi ya 58.
-
Katibu Mkuu wa UN: Mahesabu mabaya Asia Magharibi yatasababisha janga kwa dunia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu hali ya sasa katika eneo la Asia Magharibi na kusisitiza kuwa, kosa moja la kimahesabu yumkini likasababisha maafa kwa eneo hilo na dunia nzima kwa ujumla.
-
Marekani; kizuizi kikuu kwa Palestina kuwa mwanachama kamili katika Umoja wa Mataifa
Marekani ambayo ni muungaji mkono mkuu wa Israel kwa mara nyingine imetumia kura ya turufu (Veto) na kuzuia kupasishwa uanachama kamili wa Palestina ndani ya Umoja wa Mataifa.
-
Bunge la Marekani laionya Washington isijiingize kwenye vita vya kijeshi na Iran
Mkuu wa Kamati ya Kijasusi ya Bunge la Marekani amewaonya viongozi wa Washington kuhusu matokeo mabaya ya kujiingiza katika hatua yoyote ya kijeshi inayoweza kuchukuliwa dhidi ya Iran.
-
Trump, rais wa kwanza wa zamani Marekani kuhukumiwa katika kesi ya jinai
Kesi ya Donald Trump katika mashtaka ya jinai ilianza jana, Jumatatu, mjini New York na kumfanya kuwa rais wa kwanza wa zamani wa Marekani kufika mbele ya mahakama ya jinai kujibu mashtaka yanayohusiana na kulipa pesa kwa mwigizaji wa filamu za ngono ili kumnyamazisha na kumtaka afiche uhusiano wake wa kingono na mwanamke huyo.
-
Kikao cha Baraza la Usalama: Uwanja wa makabiliano kati ya waungaji mkono wa Iran na Wamagharibi wanaounga mkono utawala wa Kizayuni.
Kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kujadili mashambulizi ya Iran ya kuuadhibu utawala wa Israel kilifanyika Jumapili jioni tarehe 14 Aprili, kikao ambacho kilibadilika na kuwa uwanja wa makabiliano kati ya nchi zinazounga mkono Iran na kambi ya Magharibi waitifaki wa utawala wa Kizayuni.
-
Biden amwambia Netanyahu kwamba Marekani haitashiriki katika vita vya Israel dhidi ya Iran
Rais Joe Biden wa Marekani amemwambia Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel kwamba Marekani haitashiriki katika mashambulizi yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran.
-
Mwakilishi wa Iran UN asisitiza ulazima wa kuuadhibu utawala vamizi wa Israel
Ofisi ya Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa imesema Baraza la Usalama lilipaswa kulaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya maeneo ya kidiplomasia ya Iran huko Damascus, mji mkuu wa Syria.
-
Kansela wa Ujerumani ashinikizwa kuacha kuipatia Israel silaha
Mamia ya watumishi wa umma wa Ujerumani wameungana na harakati ya kumtaka Kansela Olaf Scholz aache kuupatia silaha utawala haramu wa Israel huku utawala huo ukiendeleza jinai zake za kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Wafanyikazi wa Google walalamikia kandarasi ya dola bilioni 1.2 na Israel
Idadi kubwa inayozidi kungezeka ya wafanyakazi wa shirika la kiteknolojia la Google wamejiunga na kampeni ya malalalmiko ya kuitaka kampuni hiyo ya Marekani kuachana na kandarasi ya dola bilioni 1.2 inayoipatia Israel huduma za kitekonolojia zinazojulikana kama Project Nimbus.
-
Waziri wa Ulinzi wa serikali ya Obama: Waisraeli kwanza wanafyatua risasi, kisha wanauliza maswali!
Waziri wa Ulinzi wakati wa utawala wa Barack Obama Rais mstaafu wa Marekani amesema kuwa haishangazi kwamba Waisraeli wamekiri makosa yao baada ya shambulio la hivi karibuni na mauaji dhidi ya watoa misaada wa kimataifa wa shirika la World Central Kitchen (WCK), kwa sababu kwa kawaida wao kwanza hupiga risasi na kisha huuliza maswali!
-
Baraza la Usalama laitisha kikao cha dharura kuhusu shambulio la Israel kwenye ubalozi wa Iran
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha kikao cha dharura cha kujadili shambulizi la kigaidi la Israel katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus Syria kikao ambacho kimeshuhudia kulaaniwa vikali Israel kwa shambulio lake hilo la kigaidii.
-
Dunia yaendelea kulaani shambulio la kigaidi la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria
Dunia imeendelea kulaani vikali sambulio la utawala haramu wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mkutano wa dharura kuhusu mgomo huo mbaya.
-
Katibu Mkuu wa UN alaani shambulio la Israel lililolenga ubalozi mdogo wa Iran Damascus
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria na kuonya kwamba mahesabu yoyote ya kimakosa yanaweza kusababisha mapigano yenye wigo mpana zaidi katika eneo hili tete na lisilo na uthabiti na kusababisha matokeo haribifu kwa raia.
-
Hatua mpya ya BRICS kufuta sarafu ya dola ya Marekani
Jumuiya ya BRICS ya mataifa yanayoibukia kiuchumi inajadili uwezekano wa kubuni mfumo huru wa malipo unaozingatia sarafu za kidijitali ili kupunguza utegemezi kwa mifumo ya fedha ya nchi za magharibi.
-
Mbunge wa Marekani ataka kadhia ya Ghaza imalizwe kama zilivyofanyiwa Hiroshima na Nagasaki
Tim Walberg, Mbunge wa jimbo la Michigan Kusini nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican amelazimika kufuta kauli aliyotoa ya kutaka Ukanda wa Ghaza uliozingirwa, ambao ni makazi ya zaidi ya watu milioni mbili, ushughulikiwe kama ilivyofanyiwa miji ya Nagasaki na Hiroshima ya Japan ambayo ilishambuliwa na Marekani kwa mabomu ya nyuklia.
-
Naibu Katibu Mkuu wa UN: Jaribio la kuitenga UNRWA lazima likome
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na uratibu wa misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za kibinadamu Ghaza, hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.
-
Licha ya kuikosoa Israel hadharani, Biden ameidhinisha kwa siri silaha mpya za kuwaulia Wapalestina
Rais Joe Biden wa Marekani hivi karibuni ameidhinisha kwa siri kupatiwa utawala wa Kizayuni wa Israel silaha mpya za kivita zenye gharama ya mabilioni ya dola zikiwemo aina za kisasa za mabomu na ndege za kivita.
-
Kupokewa vizuri ripoti ya UN kuhusu mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel huko Ghaza
Tathmini ya ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Palestina juu ya mauaji ya umati yanayofanywa na Israel kwenye Ukanda wa Ghaza imepokewa vizuri na kuungwa mkono na wawakilishi wa nchi za dunia ndani ya umoja huo.
-
UN: Huenda Israel imetenda jinai ya kivita kwa kutumia njaa kama silaha ya vita
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema hatua ya utawala wa Israel kutumia njaa kama silaha dhidi ya watu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza yumkini ikawa jinai ya kivita.
-
ICJ: Israel lazima ihakikishe msaada wa dharura, chakula vinaingizwa Ghaza bila kuchelewa
Mahakama ya Juu zaidi duniani ya Haki ICJ imeuamuru utawala wa Kizayuni wa Israel "kuhakikisha msaada wa haraka wa kibinadamu" unaingizwa huko Ghaza bila kuchelewa, ikisisitiza kuwa "njaa imeshaingia" katika eneo hilo.
-
CDC: Maambukizi ya magonjwa ya zinaa yameongezeka sana Marekani
Mambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs) yanaonekana kuongezeka kwa kiwango cha kuogofya miongoni mwa watu wazima nchini Marekani.
-
Marekani yaiwekea vikwazo GAZA NOW kwa tuhuma za kuchangisha fedha za kuisaidia HAMAS
Wizara ya Fedha ya Marekani imeiwekea vikwazo tovuti ya mtandao ya GAZA NOW kwa madai ya kuchangisha misaada ya kifedha kwan ajili ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS.
-
Guterres akiri kashfa ya kimaadili ya utawala wa Kizayuni katika kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametembelea kivuko cha Rafah (kati ya Ukanda wa Gaza na Misri), katika mwezi wa sita wa mauaji ya halaiki ya utawala wa Kizayuni huko Gaza, na kukitaja kitendo cha utawala huo wa Kizayuni cha kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza kuwa ni "kashfa ya kimaadili".