Rais wa Marekani amesema: aslimia kubwa ya waislamu hutangaza uislamu kuwa ni dini ya suluhu na amani, ama vikundi vya kigaidi vya Daesh na Alqaida si vikundi vya kwana kuwa na msimamo mkali katika historia ambapo hulitumia vibaya jina la Mungu

4 Februari 2016 - 13:06

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Rais Baraka Obama kwa mara ya kwanza katika kipindi cha utawala wake wa urais nchini Marekani amefanya ziara yake ya kuutembelea msikiti mmoja uliopo nchini humo nakupinga kauli alioitoa mgombea wa chama cha Republican dhidi ya Uislam na waislamu.
Rais wa Marekani aliyasema hayo siku ya Jumatano katika makao makuu ya kiislamu yaliopo jimbo la Maryland kuwa wakristo wanapaswa kujua kuwa kuishambulia na kuwa dhidi ya dini fulani ni sawa na kuzishambulia dini zetu zote.
Kauli ya Obama imetokea baada ya shambulio la kigaidi la kikundi cha Daesh mjini Paris na lile liliotokea katika jimbo la California ambapo mgombea urais wa mwaka 2016 kutoka chama cha Republican alitoa hutuba yake dhidi ya waislam na kuitaka serikali kuzuia kuingia waislam katika taifa hilo.
 Aidha Rais Obama katika mazungumzo yake ameashiria mazungumzo ya mgombea urais wa mwaka 2016 kutoka chama cha Republican Donald Trump yanayoitaka serikali ya Marekani kuwazuia wafuasi wa dini ya kislamu kuingia nchini Marekani amesema: mara nyingi imeonekana wananchi wa Marekani kutokana na vitendo vya kigaidi vya kikundi fulani, husababisha kuvihusisha vitendo hivyo na dini yote kwa ujumla, kiasi kwamba hata wanasiasa kulitumia vibaya suala hilo kisiasa, kitu ambacho hakina nafasi katika nchi ya Marekai.
Rais wa Marekani aliingia katika msikitni huo kama wanavyoingia waislamu ambapo alivua viatu alipokuwa anaingia katika msikiti huo kisha akasema: nataka kuwaambia maneno mawili ambayo si mara nyingi mtu kuwaambia waislamu wa Marekani: kwakweli nawashuku sana.
Naye alisema kuwa asilimia kubwa ya waislamu huutangaza Uislamu kuwa ni dini ya suluhu na amani huku akiainisha kuwa kikundi cha Daesh na Alqaida si vikundi vya kwanza vilivyokuwa na msimamo mkali ambao hutumia vibaya jina la Mungu.
Naye amesisitiza na kusema kuwa: vitendo kama hivi pia vimeshuhudiwa katika kila historia ya dini.   
 Aidha alisema kuwa kwa masikitiko makuwa vyombo vya habari vya Marekani vimekuwa vikifanya propaganda dhidi ya Uislamu, kitu ambacho kinapelekea kuzidisha chuki, vitisho na mauzi dhidi ya waislamu na kuuziwa wanawake wanaovaa hijabu nchini humo.
mwisho wa Habari/290