Taasisi ya Furqan Foundation imetoa shukrani za dhati kwa wafadhili waliowezesha mradi huu, na pia imetoa wito kwa wanakijiji kutunza na kusimamia kisima hiki, ili mradi huo uendelee kutoa manufaa ya muda mrefu na kuondoa adha ya ukosefu wa maji kama ilivyokuwa awali.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Taasisi ya Furqan Foundation imefanya ufunguzi rasmi wa kisima cha Maji Safi ya Kunywa namba 8 katika kijiji cha Mgomba, Kata ya Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, Mkoani Pwani. Kisima hiki kinatarajiwa kuhudumia zaidi ya wanakijiji 7,500 kutoka Kijiji cha Mgomba, Kata ya Ikwiriri, na maeneo jirani ya pembezoni.

Ufunguzi wa kisima huo ulihudhuriwa na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mgomba, ndugu Rehani Uweso, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali za vijiji na viongozi wa dini, walioshiriki katika hafla hiyo kwa furaha.

Your Comment