Kongamano la Kiislamu Kibaha Latoa Mafunzo ya Kina juu ya Uislamu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) +Picha
Kongamano hilo limeelezwa kuwa ni hatua muhimu ya kuimarisha uamsho wa kielimu na kiroho, huku Waandaji wakiahidi kuendelea kuratibu programu kama hizi ili kuendeleza malezi bora ya Kiislamu na kuimarisha umoja miongoni mwa Waumini.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kongamano la Kiislamu kwa Waumini wa Kiislamu limefanyika kwa mafanikio makubwa katika mji wa Kibaha, mkoani Pwani, likiwakutanisha Waumini kutoka maeneo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha elimu ya Dini na mshikamano wa Kiislamu.

Katika kongamano hilo, mafunzo mbalimbali ya kielimu na kiroho yalitolewa, yakilenga kuwaongezea Waumini uelewa sahihi wa Uislamu wao, misingi ya Imani, na wajibu wa Muislamu katika maisha ya kila siku. Wahadhiri walisisitiza umuhimu wa kushikamana na Mafunzo Matukufu ya Kiislamu kama yalivyofundishwa na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w), pamoja na kuyaishi kwa vitendo katika jamii.

Washiriki walieleza kufurahishwa kwao na maudhui ya kongamano hilo, wakibainisha kuwa limewapa motisha mpya ya kuimarisha Imani, kuongeza uelewa wa Dini, na kuendeleza maadili mema ya Kiislamu katika familia na jamii kwa ujumla.

Your Comment