Mheshimiwa Mufti aliwahimiza wanazuoni waendelee kusimamia haki, kuhubiri dini kwa hekima na subira, na kutoacha jukumu lao la kuuelimisha umma licha ya changamoto zinazowakabili.

26 Desemba 2025 - 16:55

Mufti Mkuu wa Tanzania: Mashekhe Msihofu Kutukanwa, Ni Njia ya Thawabu Siku ya Qiyama +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zuber bin Ally, amewahimiza Masheikh na wanazuoni wa Kiislamu kutokata tamaa wala kuogopa wanapokumbana na matusi na dhihaka, hususan kupitia mitandao ya kijamii. Amesisitiza kuwa matusi na dhuluma wanazopata wasimamizi wa dini ni sehemu ya safari ya kuutetea Uislamu, na kwamba Uislamu utaendelea kuwepo hadi Siku ya Qiyama.

Akizungumza katika Maulid iliyofanyika jana tarehe 24 Desemba katika Madrasa Nurul Yaqin, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mufti alisema kuwa wanazuoni wa dini wamekuwa wakitukanwa na kusumbuliwa tangu enzi za Mitume (s.a.w.w). Alikumbusha kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Mitume wote waliotangulia hawakuachwa salama, bali walikumbana na upinzani, kejeli na matusi kutoka kwa watu wao.

Mufti Mkuu wa Tanzania: Mashekhe Msihofu Kutukanwa, Ni Njia ya Thawabu Siku ya Qiyama +Picha

Mufti alieleza kuwa Masheikh hawapaswi kuona tabu au kuvunjika moyo wanaposikia wakitukanwa mitandaoni, kwani kwa kufanya subira wanajijengea thawabu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Alisisitiza kuwa matusi hayo ni sehemu ya mtihani, na kwamba kila anayevumilia kwa ajili ya dini yake, atajisafisha na kulipwa mema Siku ya Qiyama.

Mwisho, Mufti aliwahimiza wanazuoni waendelee kusimamia haki, kuhubiri dini kwa hekima na subira, na kutoacha jukumu lao la kuuelimisha umma licha ya changamoto zinazowakabili.

Mufti Mkuu wa Tanzania: Mashekhe Msihofu Kutukanwa, Ni Njia ya Thawabu Siku ya Qiyama +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha