Sheikh Abdul-Majid: "Mafanikio ya Mwanafunzi yanategemea sana upangaji mzuri wa mipango, kuweka malengo ya wazi, na kuwa na nidhamu ya kujisomea. Wanafunzi wanatakiwa kuweka vipaumbele katika majukumu yao na kupanga muda wa masomo kwa utaratibu ili kuongeza tija katika safari yao ya kielimu".
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam - Tanzania. Kikao cha kielimu chenye mada “Talaba (Wanafunzi) wa Hawza na Mbinu za Mafanikio katika Masomo” kimefanyika katika Uwakilishi wa Al-Mustafa, Dar es Salaam, kwa ushiriki wa wanafunzi wa Hawza.
Mzungumzaji Katika Kikao hiki cha Kisayansi alikuwa ni: Hujjatul-Islam wal-Muslimin, Samahat Sheikh Abdul-Majid Nasser. Katika hotuba yake, Sheikh Abdul-Majid aliwakaribisha Wanafunzi wapya (kwa mwaka wa masomo 2026) na kusisitiza umuhimu wa elimu za Hawza pamoja na njia bora na zenye ufanisi za kufanikiwa katika masomo.
Alieleza kuwa mafanikio ya mwanafunzi yanategemea sana upangaji mzuri wa mipango, kuweka malengo ya wazi, na kuwa na nidhamu ya kujisomea. Aidha, aliwahimiza wanafunzi kuweka vipaumbele katika majukumu yao na kupanga muda wa masomo kwa utaratibu ili kuongeza tija katika safari yao ya kielimu.
Kikao hicho kililenga kuwajengea Wanafunzi uwezo wa kielimu, kimaadili, na kiutendaji, ili waweze kutimiza vyema jukumu lao katika kuhudumia jamii na Uislamu kwa ujumla.
Kikao hicho kimefanyika leo hii siku ya Jumamosi, tarehe 24 Januari 2026, katika Kituo cha Kisayansi cha Uwakilishi wa Al-Mustafa, Dar es Salaam - Tanzania.
Your Comment