Sala si mzigo, bali ni ufunguo wa mafanikio kiroho na kimaisha, na Mwanafunzi anayehuisha 'Sala Tano' za kila siku na akazifanyia pupa, huyo atakuwa ameunganisha baina ya mambo mawili: Kuitafuta Dunia na Kuitafuta Akhera.

27 Januari 2026 - 22:29

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sala ni nguzo kuu ya Uislamu na ni njia ya moja kwa moja ya Muumini kuungana na Allah (SWT). Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:


"إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَوْقُوتًا"


"Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu"

[Surah An-Nisa: 103]

Mwanafunzi wa Elimu Tukufu ya Dini na Umuhimu wa Kusali Sala Kwa Wakati Wake Maalum Ulioandikwa +Picha

Kwa Mwanafunzi wa elimu Tukufu ya Dini, ambaye anajitahidi na kufanya kila liwezekanalo ili kupata maarifa na hekima, kusali kwa wakati wake maalum ni msingi wa kupanga maisha na kudumisha nidhamu.

Kusali kwa wakati wake maalum kunampa Mwanafunzi uwezo wa kuzingatia masomo yake bila kuishi maisha ya hovyo, na pia kunamfundisha uvumilivu na nidhamu, ambazo ni sifa muhimu katika safari ya elimu.

Mwanafunzi anayezingatia sala tano kila siku na akajali kuziswali  kwa wakati wake maalum, hujenga nafsi yake kwa misingi ya Taq'wa na uelewa (ufahamu) sahihi, na hivyo maarifa yake yanakuwa yenye faida kwake na kwa jamii nzima kwa ujumla.

Mwanafunzi wa Elimu Tukufu ya Dini na Umuhimu wa Kusali Sala Kwa Wakati Wake Maalum Ulioandikwa +Picha

Kwa hivyo, Sala si mzigo, bali ni ufunguo wa mafanikio kiroho na kimaisha, na Mwanafunzi anayehuisha 'Sala Tano' za kila siku na akazifanyia pupa, huyo atakuwa ameunganisha baina ya mambo mawili: Kuitafuta Dunia na Kuitafuta Akhera.

Your Comment

You are replying to: .
captcha