Dr. Baqir Ali alisisitiza: Dhana ya upinzani katika fikra za Kiislamu – umuhimu wake katika tamaduni na fikra. Upinzani wa Kiislamu na uchumi – mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi na kujitegemea kwa jamii.
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii arehe: Jumamosi, 31-01-2026 Kikao cha awali cha Mkutano wa Kimataifa wa Dhana ya Upinzani wa Kiislamu katika Sayansi za Binadamu kimefanyika kwa kuhudhuriwa na wanafunzi na walimu, katika Makao Makuu ya Uwakilishi wa Al-Mustafa, Dar es Salaam, Tanzania.

Katika kikao hiki, Mheshimiwa Dr. Baqir Ali alisisitiza hoja kuu zifuatazo:
1_Dhana ya upinzani katika fikra za Kiislamu - umuhimu na nafasi ya upinzani katika tamaduni na fikra za Kiislamu.
2_Upinzani wa Kiislamu na uchumi - nafasi ya mafundisho ya upinzani katika maendeleo ya kiuchumi na kujitegemea kwa jamii za Kiislamu.
Kikao hiki kilitoa fursa muhimu ya majadiliano, kubadilishana mawazo, na kuongeza uelewa wa kitaaluma kwa washiriki, na kuimarisha kuelewa dhana za upinzani wa Kiislamu katika fani za sayansi za binadamu.
Your Comment