Siku ya Jumatano, 18 Februari 2026, Dk. Ali Taqavi, Rais wa Chuo cha Al-Mustafa International Foundation- nchini Tanzania, alifanya mkutano na wanafunzi wa taasisi hiyo. Katika kikao hicho, alisisitiza umuhimu wa elimu yenye maadili na uwajibikaji, akahimiza kuimarishwa kwa mazingira ya masomo na mawasiliano ya karibu kati ya uongozi na wanafunzi.

18 Februari 2026 - 20:42

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Siku ya Jumatano, tarehe 18 Februari 2026, umefanyika mkutano wa somo la kiakhlaq na wenye manufaa ya Kielimu kati ya Rais wa Uwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s) nchini Tanzania, Dk. Ali Taqavi, na wanafunzi wa taasisi hiyo ya kielimu.

Katika mkutano huo, Dk. Taqavi aliwakaribisha wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2026, na kusisitiza umuhimu wa kutafuta elimu sambamba na kujenga maadili na kujitakasa nafsi. Alieleza kuwa dhamira kuu ya Chuo cha Al-Mustafa ni kulea wanafunzi wenye elimu, uadilifu na uwajibikaji kwa Umma wa Kiislamu na jamii kwa ujumla. Aidha, alibainisha nafasi muhimu ya wanafunzi katika kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s) na kuimarisha umoja wa Kiislamu.

Baada ya hotuba yake, wanafunzi walipata fursa ya kutoa maoni, mapendekezo na kuwasilisha baadhi ya changamoto za kitaaluma na kijamii. Rais wa uwakilishi alisikiliza kwa makini na kuahidi kufuatilia hoja zilizotolewa pamoja na kuboresha mazingira ya masomo, utafiti na malezi ya kiutamaduni.

Mkutano huo ulifanyika katika hali ya maelewano na mazungumzo ya wazi, na ukahitimishwa kwa msisitizo wa kuendeleza mikutano ya aina hii ili kuimarisha uhusiano kati ya uongozi na wanafunzi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha