Alhaj Dkt. Saleh Maulid, akizungumza baada ya Sala ya Dhuhri katika Chuo cha Kisayansi cha Al-Mustafa International Foundation- Tanzania, alisisitiza umuhimu wa imani na matendo mema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, akibainisha kwamba matendo mema kama usomaji wa Qur’an, sala za usiku, utoaji wa sadaka na kusaidia maskini huimarisha Taq'wa, subira, shukrani na malezi ya kiroho miongoni mwa Waumini.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kikao cha kielimu chenye anuani: “Imani na Matendo Mema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan” imefanyika Jumamosi 21/02/2026 katika Chuo cha Sayansi ya Kidini cha Al-Mustafa International Foundation- Tanzania.
Al-Haj Dkt.Saleh Maulid, Mzungumzaji wa kikao hicho kilichofanyika baada ya Sala ya Dhuhrain, alielezea umuhimu wa imani na nafasi ya matendo mema katika kuimarisha Taq'wa na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Alitaja Aya za Qur’an Tukufu, ikiwa ni pamoja na:
﴿شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ﴾ (بقره: ۱۸۵)
"Mwezi wa Ramadhan ni ule ambao Qur’an ilitumika kuwa mwongozo kwa watu na mashahidi wazi wa mwongozo na utambulisho wa mema"(Al-Baqarah: 185).
Aidha, mzungumzaji alinikia hadithi za Mtume Muhammad (saww) akisisitiza kuwa siku ya kufunga na Qur’an ni kinga dhidi ya dhambi na njia ya kukaribia Mwenyezi Mungu, huku matendo mema katika mwezi huu yakipatiwa thawabu mara nyingi zaidi.
Dkt.Saleh Maulid pia alibainisha umuhimu wa matendo mema kama vile Sala za usiku, sadaka, usomaji wa Qur’an, na utoaji wa msaada kwa maskini, akisisitiza kwamba matendo haya si tu huimarisha imani bali pia hujenga subira, shukrani na maadili mema.
Wanafunzi walihudhuria kikao hiki cha Kielimu walitoa maswali mbalimbali juu ya mada husika, na kupata majibu yakinifu kutoa kwa mtoa mada, na hatimaye kupatia mwangaza wa kielimu na kivitendo.
Your Comment