Katika khutba ya Ijumaa Malawi, Sheikh Abdul Rahman Kachere alisisitiza mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuhusu uadilifu, kujiepusha na fitna, na umuhimu wa maadili mema katika jamii ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, katika Swala ya Ijumaa iliyofanyika tarehe 12/06/2026, Khatibu Sheikh Abdul Rahman Kachere ametoa nasaha maalumu kwa waumini akisisitiza mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa masahaba wake kuhusu maadili, subira na kujiepusha na maovu ya kijamii.
Khutba hiyo ilihudhuriwa na wanafunzi na walimu wa Chuo cha Al-Hadi nchini Malawi pamoja na baadhi ya Waislamu wa Kishia wa eneo hilo.
Sheikh Kachere alieleza kuwa mafundisho ya Mtume (s.a.w.w) yanatoa mwongozo muhimu katika maisha ya kila siku, hasa katika kujenga jamii yenye uadilifu, ucha-Mungu na maadili mema. Akinukuu baadhi ya riwaya za Kiislamu, alibainisha mambo kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na:
1-Kuwa tayari kwamba kwa sababu ya kusimamia uadilifu, baadhi ya watu wanaweza kukuchukia.
2-Kujiepusha na tamaa za mwili na kusubiri ili kupata yale yaliyo bora na ya halali.
3-Kujilinda dhidi ya fitna na matamanio yanayoweza kupotosha moyo wa mtu.
4-Kukumbuka kuwa yaliyopita ni mbali, na yajayo ni karibu hivyo mtu ajitayarishe kwa akhera.
5-Kuepuka kuzungumza sana katika mambo yasiyomhusu Mola.
6-Kujiepusha na tabia ya kuwachunguza na kuwatafuta aibu za wengine kana kwamba umewekwa kuwa mlinzi wao.
Alisisitiza kuwa mafundisho haya yanapaswa kuwa mwongozo kwa waumini katika kujenga jamii yenye maadili bora na yenye kumcha Mungu.
Your Comment