Majlisi ya maombolezo ya Imam Hussein (a.s.) imefanyika kwa ushiriki wa wanafunzi Wasichana wa Hawzah ya Hazrat Zainab (sa) iliyopo Kigamboni - Dar-es-salaam. Majlisi hiyo ilijumuisha usomaji wa Qur’an na hotuba za kielimu na maarifa (juu ya Matukio ya Karbala) kutoka kwa Wanafunzi wa Chuo hicho.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Majlisi ya maombolezo ya Imam Hussein (a.s.) imefanyika siku ya Jumanne, tarehe 23/06/2026, sambamba na 8 Muharram 1447 Hijria katika Maeneo ya Kigamboni Jijini Dar-es-salaam Tanzania.
Hafla hiyo imehusisha usomaji wa Qur’an ulioongozwa na mwanafunzi Aisha Moshi pamoja na usomaji wa Qaswida na nyiradi uliofanywa na wanafunzi Aisha Miu na Arafa Hatib.
Aidha, wanafunzi Sabra na Kawthar Shahid walitoa hotuba fupi zilizoangazia mafunzo ya Karbala na umuhimu wa kusimama kwa haki, uadilifu na ujasiri katika maisha ya kila siku.
Kwa mujibu wa waandaaji na wasimamizi wa Shule ya Wasichana Kigamboni, jumla ya Wanafunzi 144 walihudhuria majlisi hiyo pamoja na wasimamizi wao ikiwa ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hussein (a.s.) na wafuasi wake katika tukio la A'shura.
Your Comment