Sheikh Jalala amesema kuwa Imam Hussein (a.s) alipigania utu wa binadamu, umoja wa Waislamu na maadili ya amani, upendo na mshikamano, akibainisha kwamba ujumbe wa Karbala unaendelea kuwa nuru ya uhuru wa fikra na haki kwa watu wote duniani.

25 Juni 2026 - 22:19

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA–, Sheikh Jalala amesema kuwa mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussein (a.s), alisimama na kujitolea mhanga katika ardhi ya Karbala kwa ajili ya kutetea utu wa binadamu, kueneza amani, upendo na kuhimiza mshikamano miongoni mwa watu.

Akizungumza katika maadhimisho ya kumuenzi na kumuomboleza Imam Hussein (a.s) yaliyofanyika Dar es Salaam, Sheikh Jalala alieleza kwamba mapambano ya Karbala hayakuwa kwa maslahi ya kundi fulani, bali yalikuwa ni harakati za kusimamisha haki, kupinga dhulma na kuimarisha umoja baina ya Waislamu na wanadamu wote.

Alisisitiza kuwa mafundisho ya Imam Hussein (a.s) yanaendelea kuhamasisha jamii kusimamia haki, kuheshimu utu wa kila mwanadamu na kujenga dunia yenye amani na mshikamano.

Washiriki wa maadhimisho hayo walieleza kuwa kumbukumbu ya Ashura ni fursa ya kutafakari thamani za kujitolea, uvumilivu na kusimama dhidi ya dhulma, huku wakisisitiza kuwa “Karbala ni njia ya uhuru wa fikra” na ujumbe wake unabaki kuwa mwanga kwa vizazi vyote.

Your Comment

You are replying to: .
captcha