Waumini na wapenzi wa Ahlul-Bayt (AS) wamefanya maandamano ya amani katika eneo la Kigogo Post, Dar-es-Salaam, kuomboleza tukio la Karbala na kusisitiza kuendeleza ujumbe wa mapinduzi ya Imam Hussein (AS).
Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maelfu ya waumini na wapenzi wa Imam Hussein (AS) na Ahlul-Bayt (AS) kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar-es-Salaam walijitokeza kwa wingi katika eneo la Kigogo Post kushiriki katika maombolezo ya Siku ya Ashura.
Shughuli hiyo ilijumuisha maandamano ya amani ya kidini yaliyolenga kuonyesha huzuni na kulaani dhulma na mauaji yaliyotokea katika tukio la kihistoria la Karbala dhidi ya mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na masahaba wake waaminifu.
Washiriki wa maombolezo hayo walisisitiza umuhimu wa kuendeleza uhai wa malengo na mafunzo ya mapinduzi ya Imam Hussein (AS), wakieleza kuwa ujumbe wa Karbala bado unaendelea kuwa mwanga wa haki, uadilifu na mapambano dhidi ya dhulma katika jamii ya leo.
Maandamano hayo yalimalizika kwa utulivu huku yakiacha ujumbe wa mshikamano, uadilifu na ufuasi wa maadili ya Ahlul-Bayt (AS).
Your Comment