Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge ameungana na waumini na viongozi mbalimbali wa kidini katika matembezi ya amani yaliyofanyika Temeke, Dar es Salaam, kwa ajili ya kuenzi shahada ya Imam Hussein (a.s) na kusisitiza ujumbe wa haki, amani, umoja na utu kwa wanadamu wote.

28 Juni 2026 - 18:51

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, ameshiriki katika matembezi ya amani ya kumbukizi ya kumuomboleza mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussein (a.s), aliyeuawa kidhulma katika ardhi ya Karbala.

Matembezi hayo yamefanyika leo, Juni 28, 2026, katika eneo la Temeke Bilal Muslim, jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa kidini waliokusanyika kuonyesha huzuni na kuenzi msimamo wa Imam Hussein (a.s) katika kupigania haki, utu na ubinadamu.

Washiriki wa matembezi hayo walisisitiza kuwa mapambano ya Imam Hussein (a.s) dhidi ya dhulma na uonevu yanaendelea kuwa chanzo cha mafunzo kwa watu wa dini na mataifa mbalimbali duniani, yakihamasisha amani, umoja na mshikamano wa kijamii.

Matembezi hayo pia yalikuwa sehemu ya kuhuisha ujumbe wa Karbala unaowataka wanadamu wote kusimama upande wa haki, kupinga dhulma na kuendeleza maadili ya upendo, uadilifu na mshikamano katika jamii.

Your Comment

You are replying to: .
captcha