Maelfu ya waombolezaji kutoka Iran na mataifa mbalimbali duniani wameendelea kufika kuanzia jana (Jumamosi) alfajiri hadi usiku ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi Sayyid Ali Khamenei, wakimkumbuka kwa unyenyekevu wake na msimamo wake wa kutetea wanyonge, hususan wananchi wa Palestina.

5 Julai 2026 - 13:04

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Maelfu ya wananchi wa Iran pamoja na wageni kutoka pembe mbalimbali za dunia wameendelea kumiminika kuanzia alfajiri (Jumamosi) hadi usiku ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi Sayyid Ali Khamenei.

Washiriki wa maombolezo hayo walijitokeza kwa wingi wakionesha hisia zao za upendo na heshima kwa kiongozi huyo, ambaye wengi walimwelezea kuwa alikuwa mtu wa unyenyekevu, mwenye kuishi maisha ya kawaida na aliyejitolea kuwatumikia watu wake.

Wengi wa waliohudhuria pia walikumbuka msimamo wake wa kuwatetea watu wanaodhulumiwa duniani, hasa wananchi wa Palestina, wakisema kuwa alisimama daima upande wa wanyonge na kudai haki zao katika medani za kimataifa.

Waombolezaji walisisitiza kuwa urithi wake wa kutetea haki, uadilifu na kuwasaidia waliodhulumiwa utaendelea kuishi katika nyoyo za watu wengi duniani.

Your Comment

You are replying to: .
captcha