Wanafunzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Al-Mustafa nchini Tanzania walifuatilia kwa njia ya matangazo ya moja kwa moja (live) kupitia mtandao ibada ya mazishi na maziko ya Ayatullah Imam Sayyid Ali Khamenei mjini Mashhad, wakionesha mshikamano na kuwapa pole wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

9 Julai 2026 - 12:42

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– wanafunzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Al-Mustafa nchini Tanzania walishiriki kwa njia ya matangazo ya moja kwa moja kupitia mtandao katika hafla ya mazishi na maziko ya Ayatollah Imam Sayyid Ali Khamenei (ra) iliyofanyika Mjini Mashhad, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wanafunzi wa Jamiat AlMustafa(s)Tanzania Washiriki Mazishi ya Ayatollah Imam Sayyid Ali Khamenei(ra) Wakifuatilia Moja kwa Moja Kupitia Mtandao+Picha

Washiriki hao walifuatilia kwa umakini shughuli zote za mazishi na kutoa salamu za rambirambi, huku wakionesha mshikamano wao na wananchi wa Iran katika kipindi hiki cha maombolezo.

Wanafunzi hao walisisitiza kuwa ushiriki wao katika tukio hilo ni ishara ya udugu wa Kiislamu, umoja wa Umma na kuthamini nafasi ya viongozi wa dini katika kuimarisha maadili, elimu na mshikamano wa Waislamu duniani. Aidha, waliwaombea marehemu rehema na daraja ya juu mbele ya Mwenyezi Mungu pamoja na kuwatakia subira na ustahimilivu wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Your Comment

You are replying to: .
captcha