Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

11 Februari 2022

11:47:13
1228353

Wairan leo wanaadhimisha miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Leo Ijumaa tarehe 22 Bahman, sawa na tarehe 11 Februari, wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanaadhimisha sherehe za miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika sherehe hizo mamilioni ya wananchi wa taifa hili watamiminika mabarabarani katika maandamano ya amani ya kumbukumbu ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu, ambapo kwa mara nyingine watajadidisha kiapo cha utiifu kwa Imamu Khomein, Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Kadhalika Wairan watatangaza utiifu wao kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewataka wananchi wa Iran kujitokeza kushiriki katika maandamano ya maadhimisho ya miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran sambamba na kulinda miiko ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa, wananchi wa Iran wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya leo ili kuwaonyesha walimwengu wote adhama na ukubwa wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyopata ushindi mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini na kuhitimisha utawala utawala wa Shah uliokuwa ukiungwa mkono na madola ya Magharibi.

Ikumbukwe kuwa, miaka 43 iliyopita katika siku kama ya leo Iran ilikuwa katika siku ya kihistoria itakayokumbukwa siku zote. Siku hiyo wananchi waliokuwa wakipiga takbira na kutoa nara za kimapinduzi chini ya uongozi wa Ayatullah Ruhullah Khomeini walihitimisha kipindi cha giza totoro katika historia ya Iran kwa kuung'oa madarakani utawala wa kidikteta wa Shah Pahlavi. Wananchi wanamapinduzi wa Iran, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee na watu wa matabaka yote walisimama kidete wakipambana na mizinga na vifaru vya jeshi la Shah na kujisabilia kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu. 

342/