Hujjatul Islam Yusuf Al-Nasseri, mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Dini la Iraq, alitoa maelezo hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa mtandaoni (webinar) uliopewa jina la “Nasra Kutoka Kwa Allah (Nasrun min Allahi) na Mustakabali wa Muqawama.
Kikao hicho kiliandaliwa kwa pamoja na Kituo cha Utafiti wa Sayansi ya Siasa na Kituo cha Ustaarabu na Mafunzo ya Jamii siku ya Jumapili.
Al-Nasseri amesema Wamagharibi wanashuhudia waziwazi kuporomoka kwa ustaarabu wa Kimagharibi hivi leo huku wale wanaodhulumiwa wakizidi kupata nguvu na harakati ya muqawama inastawi na kuwa na nguvu zaidi huku watu wengi zaidi wakijiunga nayo siku baada ya siku.
Alisema dunia ya sasa imegawanyika kati ya harakati ya haqi na harakati ya batili na kila mtu anaweza kuutofautisha kati ya pande hizo mbili kwa urahisi.
Harakati ya haki ni ile inayowatetea wanyonge dhidi ya mabeberu, aliongeza.
Msomi huyo wa Iraq alitaja mauaji ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah Sayyidd Hassan Nasrallah na utawala wa Kizayuni na kusema washirika wa jinai hiyo ni wale wale waliomuua kamanda wa Iran, Luteni Jenerali Qassem Soleimani.
Pia alisema vita vya leo si dhidi ya makafiri na washirikina pekee bali ni vita dhidi ya wanafiki, hivyo ni vita vigumu zaidi.
Al-Nasseri amesema kimya cha baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu mbele ya ukatili wa utawala ghasibu wa Israel si chochote ila ni unafiki na kuongeza kuwa watu hao wanadhoofisha harakati ya haki kwa ukimya na unafiki wao.
Hii ni wakati sio mataifa ya Kiislamu pekee, bali mataifa ya Magharibi yanasimama dhidi ya Wazayuni na mabeberu wa kimataifa, aliendelea kusema.
Aidha amesema vita dhidi ya utawala ghasibu wa Israel havipaswi kuendeshwa na makundi ya muqawama pekee bali nchi za Kiislamu pia zinapaswa kutangaza vita dhidi ya utawala huo ghasibu.
IQNA

Wasomi kadhaa wa kidini na maprofesa wa vyuo vikuu kutoka Iran, Iraqi, Lebanon na Tunisia pia walihutubia warsha hiyo ya mtandaoni Jumapili.