Ulyanov amesema hayo wakati akitoa majibu madhubuti kwa mwandishi wa habari wa BBC ya Kiajemi ambaye alitaka kutilia shaka mpango wa amani wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa shirika la sabari la Mehr, Ulyanov ameitaja Iran kuwa jirani na mshirika muhimu wa Russia, akisisitiza kwamba urutubishaji wa madini ya urani wa Iran, hata ukifikia asilimia 90, ni wa amani kabisa.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Russia amesisitiza kuwa, Israel haina haki ya kuzungumzia miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani au kuingilia suala hilo.
Kadhalika Ulyanov amekosoa vikali vitisho vya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani vya kuamilisha mchakato wa kurejesha vikwazo dhidi ya Iran na kutaja msimamo huo kuwa wa "kutowajibika" na "ulio kinyume cha sheria".
Amebainisha kuwa, baada ya kukiuka majukumu yao chini ya azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na makubaliano ya JCPOA, nchi hizo tatu za Ulaya zinapania kuiadhibu Iran kwa tuhuma za kutoheshimu makubaliano ambayo wao wenyewe waliyavunja mnamo Agosti 2022.
342/
Your Comment