Kwa mujibu wa shirika la habari la TASS, Dmitry Peskov, msemaji wa Kremlin, ameyataja matamshi ya Volodymyr Zelensky kuhusu kufanya uchaguzi nchini humo kuwa ni ya kujipinga. Peskov alisema: "Zelensky anasema hatamruhusu Putin kuingilia uchaguzi, lakini wakati huo huo anaomba msaada wa Wamarekani kufanya uchaguzi huo."
Aliongeza kuwa hii ina maana Zelensky hana pingamizi na kuingilia kati kwa Marekani, lakini anapinga Urusi, jambo ambalo ni ishara ya kuchanganyikiwa. Muda wa urais wa Zelensky uliisha Mei 20, 2024, lakini Kyiv imekataa kufanya uchaguzi kwa kisingizio cha sheria ya kijeshi.
Your Comment