22 Desemba 2025 - 14:34
Source: ABNA
Gazeti la Ujerumani: Magharibi inajiandaa kwa shambulio la mtandaoni dhidi ya Urusi

Gazeti la Ujerumani limeripoti kuwa wadukuzi wa Ulaya wanajiandaa kufanya shambulio kubwa la mtandaoni (cyber attack) dhidi ya miundombinu ya Urusi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu Russia Today na gazeti la Ujerumani la "Die Welt", wadukuzi wanaofanya kazi kwa niaba ya mamlaka za nchi za Ulaya wamefahamisha kuwa nchi za Magharibi zinaandaa kwa siri mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya miundombinu ya Urusi.

Gazeti hilo linaongeza kuwa serikali za Magharibi hazizingatii tu ulinzi wa mtandaoni, bali zimegeukia kufanya shughuli za kishambulizi, ikiwa ni pamoja na kupenya kwenye kompyuta za ndani nchini Urusi na kuweka programu hasidi (malware) kwa siri.

Die Welt imeashiria kufanyika kwa mazoezi kuhusu suala hili katika kituo cha NATO nchini Estonia na kusema kuwa wanajeshi wa NATO wanapewa mafunzo ya kufanya operesheni kubwa katika ulimwengu wa kidijitali, ambapo miongoni mwa malengo ni mifumo ya usambazaji nishati.

Your Comment

You are replying to: .
captcha