2 Machi 2026 - 15:54
Source: IQNA
Imam Khamenei ameuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Marekani na Israel

Kufuatia shambulio la kikatili la utawala wa Kizayuni na Marekani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameuawa shahidi.

Ifuatayo ni taarifa kufuatia tukio hilo chungu.

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ ۖ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ ۖ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا

Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.

Kufuatia shambulio la kikatili la utawala wa Kizayuni na Marekani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameuawa shahidi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran ameuawa shahidi katika eneo lake la kazi, katika (Idara ya Uongozi) katika shambulio hili lisilo la kibinadamu lilitokea mapema asubuhi ya Jumamosi.

Vyombo vya habari vinavyohusishwa na utawala wa Kizayuni na madola vibaraka  mara kwa mara vilikuwa vinadai kuwa, kwa sababu ya hofu ya kuuawa, Kiongozi Muadhamu anaishi katika eneo salama na mafichoni.

Kufa kwake kishahidi katika eneo lake la kazi kumeonesha tena jinsi madai hayo na vita vya kisaikolojia vya adui vilivyokuwa havina ukweli, na kumeonyesha kuwa yeye alisimama bila woga na kwa ushujaa dhidi ya ubeberu na uistikbari akiwa kati ya watu na katika ngome ya uwajibikaji.

Baraza la Mawaziri la Serikali ya Iran limetangaza maombolezo ya kitaifa kwa siku 40 na likatangaza likizo ya kitaifa kwa siku 7.

Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, katika mahojiano ya televisheni leo asubuhi amesisitiza kuwa: “Leo, Baraza la Muda la Uongozi litaundwa kulingana na Katiba ili Kiongozi anayefuata aweze kuchaguliwa.”

Ameongeza: “Kwa mujibu wa Ibara ya 110 ya Katiba, iwapo nchi haitakuwa na Kiongozi Muadhamu kwa sababu yoyote ile, Rais wa Jamhurii, Mkuu wa Idara ya Mahakama Kuu , na mwanazuoni Faqihi kutoka Baraza la Walinzi wa Katiba, atakayeteuliwa na Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo, watachukua kwa muda majukumu ya Uongozi hadi Kiongozi anayefuata atakapochaguliwa. Hatua hii itachukuliwa haraka iwezekanavyo, na leo juhudi za kuunda Baraza la Muda la Uongozi kwa mujibu wa Katiba zinaendelea kufuatiliwa.”

Your Comment

You are replying to: .
captcha