Katika ujumbe alioutoa siku ya Jumapili, Ayatullah Mkuu Nasser Makarem Shirazi aliwataka mataifa ya Kiislamu, watu huru wa ulimwengu, na serikali za Kiislamu kusimama pamoja kuwasaidia wananchi wa Lebanon wanaokabiliwa na hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel wakiwa pamoja na wanamapambano hodari na jasiri wa Hizbullah
Amesema: “Habari za mashambulizi makali ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye sehemu mbalimbali za Lebanoni na mauaji ya mamia ya watu wasio na hatia, hasa wanawake na watoto, zimeleta huzuni na majonzi makubwa.”
Ameongeza: “Bila shaka, utawala huu ambao hauna heshima kwa misingi ya ubinadamu umetekeleza uhalifu unaoumia dhamiri ya kila mtu huru kwa kushambulia hospitali, miundombinu muhimu na maeneo ya raia.”
Ayatullah Makarem Shirazi amesisitiza:
“Ni wajibu kwa mataifa ya Kiislamu, watu huru wa ulimwengu na serikali za Kiislamu kusimama pamoja kuwasaidia watu wasio na ulinzi wa nchi hii na wapambanaji wa Hizbullah. Uzoefu wa nyuma umeonyesha kuwa udhaifu au kujisalimisha mbele ya uchokozi kunafungua mlango wa kurudiwa kwa mashambulizi na kuongeza ukubwa wake.”
Aidha, kiongozi huyo aliongeza kuwa:
“Inatarajiwa kuwa taasisi na viongozi husika wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kama walivyofanya hapo awali, wataendeleza juhudi zao kwa mujibu wa wajibu wa kibinadamu na Kiislamu ili kupunguza mateso na kuwasaidia watu wa Lebanoni wanaodhulumiwa.”
Mwishoni mwa ujumbe wake, Ayatullah Makarem Shirazi alitoa rambirambi zake kwa Imam Zaman (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake) kwa tukio hili lenye uchungu mkubwa, na akaomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awainue daraja za mashahidi, awaponye haraka waliojeruhiwa, na awape subira pamoja na ujira wale waliobaki hai.
Your Comment