-
Nafasi ya Mwanamke katika Harakati ya Mabadiliko ya Imam Hussein (a.s) | Madrasat Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni - Dar-es-salaam + Picha
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majlisi ya Siku ya 6 ya Maombolezo ya Shahadat ya Imam Hussein (as) imefanyika katika Madrasat ya Wasichana wa Kiislamu ya Hazrat Zainab (sa), iliyopo Kigamboni Jijini Dar-es-salaam. Ushiriki Mzuri wa Mabanati wa Kiislamu katika kuhuisha Ujumbe wa Mapinduzi ya Imam Hussein (as), ni katika muendelezo wa ukweli ule halisi kwamba Mwanamke wa Kiislamu alikuwa mshirika wa msingi katika kuendeleza na kuhifadhi mafanikio ya harakati ya Imam Hussein (a.s). Kwa maana kwamba: Uwepo wa Wanawake katika tukio la Karbala haukuwa wa bahati (au wa kubahatisha) au jambo la ghafla, bali ulikuwa sehemu ya mpango wa kimkakati uliopangwa na Imam Hussein (a.s) mwenyewe - ili kuonyesha ulimwengu kuwa Mwanamke ana nafasi ya kuchukua maamuzi muhimu na kuyatetea kwa ujasiri mkubwa.