Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Kundi kubwa la waandamanaji maarufu wamelaani jinai ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni katika mauaji ya Syed Hassan Nasrullah, na kusisitiza uungaji mkono wao kwa mataifa ya Lebanon na Palestina.

29 Septemba 2024 - 20:22
Washiriki wa maandamano hayo ya hadhara waliutaja utawala wa Kizayuni kuwa ni "dola la kigaidi" na wakiwa wamebeba mabango ya kuomboleza kuuawa Shahidi Marhumu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hezbollah ya Lebanon. Maandamano haya ya maelfu ya watu yalifanyika katika ukumbi wa jiji la Sydney na Melbourne nchini Australia.