Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - ABNA - Hafla ya uzinduzi wa Tafsiri ya Qur'an Tukufu kwa Lugha ya Kiswahili iliyoandikwa na Marehemu Sheikh Hassan Ali Mwalupa (Mwenyezi Mungu Amrehemu) imefanyika nchini Tanzania. Wafuasi wa Madhehebu mbalimbali za Kiislamu nchini Tanzania, wakiwemo Mashia wa Khoja wa nchi hii ni miongoni mwa waliohudhuria katika hafla hii.

19 Machi 2025 - 14:32

Your Comment

You are replying to: .
captcha