Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Waumini na wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s) Jijini Arusha, Tanzania, wamehuisha Usiku Mtukufu wa wa 19 wa Ramadhan katika Husseiniyya ya Imam Ridha (as). Usiku huu ndio Usiku ambao Amirul Muuminina Ali (a.s) alipigwa upanga kichwani akiwa ndani ya Msikiti na akiswali Swala ya Al-fajiri. Laana iwe juu ya Ibn Muljim aliyefanya tukio hili lenye kuziumiza nyoyo za Waumini. Katika picha ni Mkesha wa Kwanza wa Lailatul-Qadr ambao umeambatana na Dua mbalimbali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
20 Machi 2025 - 17:43
News ID: 1543888
Your Comment