Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (AS) - Abna-: Usiku wa Lailatul-Qadr ni Usiku ambao hakuna Usiku mwingine katika mwaka mzima unaofikia ubora wake, na kitendo cha usiku wa Lailatul-Qadr kinakuwa ni bora zaidi kuliko kitendo cha Miezi elfu moja. Katika Usiku wa Lailatul-Qadr, mipango (makadirio) ya kila mtu kwa mwaka mzima inatathminiwa (nakupangwa au kukadiriwa). Katika Usiku wa Lailatul-Qadr, Malaika na Ruhu, ambaye ni Malaika mkubwa zaidi, kwa idhini ya Mola, humtumikia (huwa katika khidma kwa) Imam wa Zama (a.t.f.s), ambapo hushuka na kuwasilisha hatima (makadirio au) ya kila mtu kwa Imam (a.t.f.s).
23 Machi 2025 - 17:08
News ID: 1544405
Your Comment