Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Sambamba na Siku za Baraka za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ikiwa ni kwa mwaka wa tano mfululizo, na kupitia juhudi za kikundi cha Tablighi cha Jihadi cha Shahidi Muhammad Reza Shafi'i, mikusanyiko ya duru za usomaji wa Qur'an Tukufu zinazohudhuriwa na wanaumena wanawake wanaofunga saumu ya Ramadhani, zimekuwa zikifanyika katika Bustani, bila kusahau uwepo wa watoto na vijana, ambapo huambatana na programu maalum zinazojiri katika Bustani hizo, katika Mji wa Qom. Program hii inaendelea hadi mwisho wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan. Bustan kama vile: Narges (Mji mdogo wa Mahdiyeh wa Wanafunzi), Saba (Nirugah, Javad Al-Aimeh), Taravat (Pardisan), Ostad Shahryar (Nirugah), Haram ya Mashahidi wa Mlima wa Khidhri Nabi (amani iwe juu yake), Shahid Mahmoodabadi (Tavanir), Shahidi Shahid Bun'yadiy (Khakfaraj), Nukhbogan (Pardisan), Hafez (Nirugah), Hashemi (Bajek), Banafsheh (Barabara ya Shahid Karimi) na Shahidi Zeinuddin (Bon'yad), zinajumuishwa katika mpango wa kufanya mikutano na mikusanyiko ya enzi ya Qur'an katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani 2024 - 2025.

26 Machi 2025 - 03:28

Your Comment

You are replying to: .
captcha