Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s); Bilal Muslim Tanga Mjini imefanya Mashindano ya Qur'an Tukufu katika vipengele :Taj'wid, Tartili, Hifdhi Juzuu 15, na Juzuu 5, na Juzuu 2, na Juzuu 1. Mashindano yalijumuisha Maarif al-Qur'an (Tafsiri ya Surat Al-Hujurat, na Surat AI-Insan). Washiriki katika mashindano hayo ni: Wanafunzi (Wavulana) wa Hawzat al-Qaim (atfs), Wanafunzi (Wasichana) wa Hawzat Al-Zahra (s.a), Waumini (jinsia zote), Wanafunzi wa Madrasa (jinsia zote). Pia mashindano hayo yamehudhuriwa na wageni mbali mbali wakiwemo viongozi wa Serikali na Kidini. Shukran za dhati ziende kwa Mudiru wa Hawza,Samahat Sheikh Kadhim kwa kupangilia na kufanikisha mashindano haya. Pia shukran za dhat ziende kwa uongozi wa Bilal Muslim Tanga Mjini kwa kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha mashindano haya ya Quran Tukufu yanafanyika. Qur'an ni nuru, na ni Kiongozi wa Maisha yetu.

26 Machi 2025 - 18:42

Your Comment

You are replying to: .
captcha