Kwa Mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan amejumuika na Waisalamu wote na Viongozi mbali mbali akiwemo Rais wa awamu ya Nne Mh.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Nchini, Mh.Mohamed Mchengerwa na wengine, kwa ajili ya kuswali Swala ya Eid -ul- Fitr, katika Msikiti wa Mfalme Mohamed wa VI uliopo Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Kinondoni, Jijini Dar es Salaam Tanzania. Swala hiyo ya Eid al-Fitr imeswaliwa leo tarehe 31 Machi, 2025.

31 Machi 2025 - 12:54

Habari Pichani | Rais wa Tanzania na Viongozi wa Kadhaa wa Serikali wajumuika na Waislamu Tanzania katika Swala ya Eid -ul- Fitr

Your Comment

You are replying to: .
captcha