Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Waumini, Wafuasi na Wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s) Jijini Arusha-Tanzania, walikutana na kusalimiana na kujumuika katika picha ya pamoja, na kufurahi kwa pamoja katika mshikamano wa Kiislamu sambamba na sherehe za kusherehekea Siku Kuu ya Eid - Al-Fitr.

4 Aprili 2025 - 19:10

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake):

قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ:

"وَاَلَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لاَ تدخلوا تَدْخُلُونَ اَلْجَنَّةَ حَتَّى تُؤْمِنُوا وَ لاَ تؤمنوا تُؤْمِنُونَ حَتَّى تَحَابُّوا أَ وَلاَ أَدُلُّكُمْ عَلَى شَيْءٍ إِنْ فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُمْ، أَفْشُوا اَلسَّلاَمَ بَيْنَكُمْ".

Habari Pichani | Waumini, Wafuasi na Wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s) Jijini Arusha-Tanzania, wakisalimiana na kujumuika katika picha ya pamoja

"Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, hamtaingia Peponi mpaka muamini, na hamtaamini mpaka mpendane. Je, niwaelekeze kwenye jambo ambalo mkilitenda mtapendana (na kujenga urafiki baina yenu)?; Enezeaneni salamu baina yenu (yaani: Toleaneni Salam ya kutakiana amani ambayo ndio kauli mbiu rasmi ya salam ya kiislamu)".

Your Comment

You are replying to: .
captcha