Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Waumini wengi wa Kiislamu wamehudhuria kwa hamasa kubwa katika Ukumbi wa Lamada Hotel - Ilala, Dar-es-salaam - Tanzania, ili kusikiliza Qaswida ya mbalimbali za Kumsifu Mtume Muhammad (saww) na kuonyesha Mapenzi Yao makubwa juu yake. Qaswida hizo zilisomwa Mubashara kwa Sauti nzuri na zenye Mahadhi mbalimbali ya Kiushairi. Qaswida zote ziliwakonga nyoyo Waislamu, ni pamoja na Qaswida ya: "Haya tumpendeni Nabiyyah"... Mahaba ya Amini hayazuiliki nyoyoni. Ametuathiri Sana Nabiyyah nyoyoni. Sote twataraji kwako kupata Shifaa yako". Qaswida hii imewakonga nyoyo Waislamu wengi Tanzania wenye Mapenzi makubwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Qaswida hii zingine nyingi zilisomwa na kundi la Qaswida la Ahlu - Zaman 2025.
10 Aprili 2025 - 21:36
News ID: 1548315
Your Comment