Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Tamasha la 30 la Kimataifa la Al-Mustafa la Quran na Hadithi - Zanzibar, limefanyika kwa mafanikio makubwa chini ya uongozi na usimamizi wa Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa, Tanzania - Dr. Ali Taqavi. Wanafunzi wa Jamiatul-Mustafa - Tanzania na vyuo vingine wameshiriki katika Mashindano haya ya Hifz ya Quran Tukufu na Hadithi. Hii ni katika kuhuisha utajo wa Quran Tukufu na hii ni harakati muhimu ya kuthamini na kuenzi Quran Tukufu inayoendelea nchini Tanzania, chini ya Uongozi bora wa Hojjat Al-Islam Dr. Ali Taqavi (Mwenyezi Mungu amuhifadhi) kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika uwanja Tablighi, kwa hakika anajituma na kuhakikisha kuwa nuru ya elimu na maarifa ya Quran na ahlulbayt (as) vinazidi kuwaangazia watu wa jamii mbalimbali nchini Tanzania.
13 Aprili 2025 - 20:15
News ID: 1548927
Your Comment