Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Siku ya Al-Quds ni wakati ambao tunapaswa kuwaonya Mataifa ya Uistikbari Ulimwenguni dhidi ya Palestina na Wanadamu wote wanaodhulumiwa, na wenye nia ya kuwadhibiti Waislamu na Uislamu na kuutokomeza kabisa, ya kwamba Uislamu hautadhibitiwa tena na nyinyi kupitia mawakala wenu waovu na wamwagaji damu katika eneo la Mashariki ya Kati. Jamiat Al-Mustafa (S), Dar -es-Salam - Tanzania, inaichukulia Kila Siku ipitayo kuwa ni Siku muhimu kwa ajili ya Quds, bali inafaa Kila Siku kuitwa kuwa ni Siku ya Quds. Katika muktadha huu, Jamiat al-Mustafa (S), Dar-es-Salam - Tanzania", chini ya Kiongozi wake Mkuu Hojjat Al-Islam wal Muslimin, Dr. Ali Taqavi, ilifanikiwa kuratibu Mkutano wa Kisayansi kwa anuani hii:"Umoja wa Waislamu Katika Kivuli cha Quds".
Alhamdulillah, Mkutano huu wa Kisayansi kuhusiana na Quds (Yerusalemu), ulifanyika kwa mafanikio makubwa ambayo ni pamoja na kuendeleza uhusiano wa kihistoria kati ya Waislamu wa Shia na Sunni nchini Tanzania, na hatimaye kufungua fursa mpya za maendeleo na mshikamano wa pamoja katika kutetea Matukufu ya Kiislamu na kusimama pamoja na Wananchi Madhulumu wa Palestina. Na hapana shaka kwamba Mkutano kama huu ni wenye kutoa matundo yake kila wakati.
Your Comment