Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlu-Bayt (a.s) - ABNA - Hawza ya Imam Zainul - A"bidina (a.s) nchini Burundi inaendelea na harakati zake za Kielimu na Utamaduni wa Kiislamu. Katika picha ni moja ya Harakati za Kielimu na Kitamaduni zinazoendelea kila siku katika Hawza ya Zainul - A'bidina (a.s) - iliyopo Burundi ambapo kila siku Wanafunzi hujipanga katika mistari na kusoma Dua mbalimbali za kila siku, katika picha ni tukio la kusoma Dua ya Siku ya Alkhamisi (kama inavyoonekana hapo chini katika Maandidhi na Audio kwa sauti ya Aba Dhar Al-Halawaji).
Utamaduni wa Kiislamu ni neno au usemi ambao mara nyingi hutumiwa kuelezea maonyesho yote ya kitamaduni na ustaarabu ambayo ni ya kawaida na ya kihistoria yanayohusishwa na Waislamu duniani kote. Mojawapo ya ufafanuzi muhimu zaidi wa utamaduni wa Kiislamu ni sayansi (elimu) ambayo inachanganya misingi ya kisheria na ufahamu halisi wa historia ya umma, na wakati wake wa sasa na wa baadaye. Tunaposema Utamaduni wa Kiislamu inamaanishwa: Kujua vipengele vya jumla vya Umma wa Kiislamu na mwingiliano wake katika siku za nyuma (zilizopita) na za sasa, ikiwa ni pamoja na dini, lugha, historia, ustaarabu, maadili na malengo jumuishi.
Mwenyezi Mungu anasema:
﴿ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ﴾ (غافر: 60)
"Niombeni Nitakujibuni" (Surah Ghafir" / Aya ya 60)"
Dua ya Siku ya Alkhamisi
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ، الْحَمْدُ لِلّٰهِ الَّذِى أَذْهَبَ اللَّيْلَ مُظْلِماً بِقُدْرَتِهِ، وَجَاءَ بِالنَّهَارِ مُبْصِراً بِرَحْمَتِهِ، وَكَسَانِى ضِياءَهُ وَأَنَا فِى نِعْمَتِهِ . اللّٰهُمَّ فَكَمَا أَبْقَيْتَنِى لَهُ فَأَبْقِنِى لِأَمْثالِهِ، وَصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ مُحَمَّدٍ وَآلِهِ، وَلَا تَفْجَعْنِي فِيهِ وَفِي غَيْرِهِ مِنَ اللَّيالِى وَالْأَيَّامِ، بِارْتِكَابِ الْمَحَارِمِ، وَاكْتِسَابِ الْمَآثِمِ، وَارْزُقْنِى خَيْرَهُ، وَخَيْرَ مَا فِيهِ، وَخَيْرَ مَا بَعْدَهُ، وَاصْرِفْ عَنِّى شَرَّهُ، وَشَرَّ مَا فِيهِ، وَشَرَّ مَا بَعْدَهُ، اللّٰهُمَّ إِنِّى بِذِمَّةِ الْإِسْلامِ أَتَوَسَّلُ إِلَيْكَ، وَبِحُرْمَةِ الْقُرْآنِ أَعْتَمِدُ عَلَيْكَ، وَبِمُحَمَّدٍ الْمُصْطَفىٰ صَلَّى اللّٰهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ أَسْتَشْفِعُ لَدَيْكَ.
فَاعْرِفِ اللّٰهُمَّ ذِمَّتِىَ الَّتِى رَجَوْتُ بِهَا قَضَاءَ حَاجَتِى، يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ، اللّٰهُمَّ اقْضِ لِىفِى الْخَمِيسِ خَمْساً لَايَتَّسِعُ لَها إِلّا كَرَمُكَ، وَلَا يُطِيقُها إِلّا نِعَمُكَ، سَلَامَةً أَقْوىٰ بِهَا عَلَىٰ طَاعَتِكَ، وَعِبادَةً أَسْتَحِقُّ بِها جَزِيلَ مَثُوبَتِكَ، وَسَعَةً فِى الْحَالِ مِنَ الرِّزْقِ الْحَلَالِ، وَأَن تُؤْمِنَنِى فِى مَوَاقِفِ الْخَوْفِ بِأَمْنِكَ، وَتَجْعَلَنِى مِنْ طَوَارِقِ الْهُمُومِ وَالْغُمُومِ فِى حِصْنِكَ، وَ صَلِّ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَآلِ مُحَمَّدٍ، وَاجْعَلْ تَوَسُّلِى بِهِ شَافِعاً، يَوْمَ الْقِيامَةِ نَافِعاً، إِنَّكَ أَنْتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ.
Sikiliza Dua hii ya Siku ya Alkhamisi ikisomwa kwa Sauti nzuri Aba Dhar Al-Halawaji katika "Audio" tuliyokuwekea hapo chini
Your Comment