Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul- Bayt (a.s) - ABNA - Dr. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) yupo katika harakati muhimu za kuandaa Hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayofanyika nchini Tanzania ikijumuisha Tanzania bara na Zanzibar. Katika picha hizi ni tukio za kukagua na kutembelea uwanja mkubwa wa michezo Jijini Dar-es-Salam - Tanzania, ambao utatumika kwa ajili ya hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayohudhuriwa na timu kubwa ya wasomaji mahiri wa Qur'an Tukufu kutoka katika nchi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

17 Aprili 2025 - 17:46

Maadalizi ya Hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayojumuisha timu mbalimbali za Wasomaji wa Qur'an wa Tanzania, Zanzibar na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliteremsha Qur'an Tukufu kwa watu ili kuwaamsha na kuwahuisha kutokana na upotofu na ufisadi ambao walitumbukia katika Enzi ya Ujahilia. Qur'an Tukufu inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuwahuisha watu kila wanapopotea na kuharibika tena baada ya kukengeuka. Kwa hiyo, uamsho na uhuishaji wa Qur'an katika vifua vyetu ni muhimu sana kwa maisha ya viumbe, na hasa kwa Wanadamu. Hafla kubwa kama hizi zinalengo la kuipa nafasi kubwa Qur'an Tukufu iendelee kutuangazia katika maisha yetu na kutuongoza katika yale yaliyokuwa mema na mazuri.

Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Qur'an Tukufu: 

إِنَّ هَٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا 

Hakika hii Qur-aani inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa. (Suratul israa Aaya 9).

Maadalizi ya Hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayojumuisha timu mbalimbali za Wasomaji wa Qur'an wa Tanzania, Zanzibar na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Your Comment

You are replying to: .
captcha