Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Ushirikiano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika muktadha wa kubadilishana ujuzi na maarifa katika kazi hii muhimu ya zimamoto na uokoaji. Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji kutoka nchini Iran alifika nchini Tanzania na kutembelea Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilicho Temeke, Jijini Dar-es-Salam - Tanzania. Samahat Sheikh Rajab Mgereza alisaidia kutarjumu Lugha ya Kiajemi kwenda Lugha ya Kiswahili na kurahisisha mawasiliano ya majeshi haya mawili ya Zimamoto na Uokoaji ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maisha ya Mwanadamu ni Maisha ya Ushirika baina ya Mwanadamu na Mwanadamu. Ushirika ni hitaji muhimu sana kwa Mwanadamu.
Maisha ya Mwanadamu ni Maisha ya Ushirika baina ya Mwanadamu na Mwanadamu. Ushirika ni hitaji muhimu sana kwa Mwanadamu.
Your Comment