Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt (a.s) – ABNA – Mufti wa nchi ya Burundi ametembelea Ofisi ya uwakilishi wa Jamiatul Mustafa(s) katika Jiji la Dar -es- Salam, Tanzania, na kukutana na kufanya mazungumzo na Hojjatul Islam wal Muslimin, Dr. Ali Taqavi. “Sheikh Ndikumagenge Masoud,” Mufti Mkuu wa Burundi, katika mkutano huu alisisitiza juu ya umoja wa Umma wa Kiislamu na alieleza matumaini yake kwamba kupitia mazungumzo na ushirikiano kati ya taasisi za kielimu na wanazuoni wa madhehebu mbalimbali, umoja katika Umma wa Kiislamu utaimarika. Hojjatul Islam Taqavi, akisisitiza juu ya ushirikiano na kuunganisha nguvu na taasisi za kidini na kielimu, alisema: Vikao hivi ni vya thamani kubwa na vitafungua njia mpya, na moja ya malengo ya ushirikiano huu ni kueneza maarifa ya Qur’an Tukufu na kuimarisha mafundisho ya Dini Tukufu ya Kiislamu.

23 Aprili 2025 - 15:14

Mufti wa Burundi wa Madhehebu ya Ahlu-Sunna,Sheikh Ndikumagenge Masudi amtembelea Rais wa Jamiat Al-Mustafa(s), Dar-es-Salam, Tanzania, Dr. Ali Taqavi

Your Comment

You are replying to: .
captcha