Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Uongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania -JMAT - (W) Busega, ukiongozwa na Mwenyekiti Sheikh Hassan Ibrahim Jafari, pamoja na Naibu Mwenyekiti wake, walifanikiwa leo hii kufanya Ziara ya kikazi ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya kikatiba.
Lengo la ziara hii lilikuwa ni kuendelea kutoa elimu na kuteua Viongozi katika ngazi ya Kijiji ili kuhakikisha Jumuiya yetu inafika hadi vijijini.
Ziara hii ilifanyika katika kata ya Malili, ambapo tulijiunga na Afisa Mtendaji wa Kata, Maafisa wa vijiji, na Viongozi wa Kidini na Kitamaduni.
Zaidi ya hayo, baada ya kutoka katika kata ya Malili, Viongozi hawa wa JMAT walielekea katika Kata ya Kalemela.
Katika picha, Viongozi wanaonekana namna walivyokutana na Viongozi wa Kidini na Afisa Mtendaji wa Kata, ambapo walitumia fursa hiyo kuendelea kutoa elimu kuhusu JMAT, ili kuhakikisha kuwa wanalisogelea lengo tukufu na maridhawa la kuongeza wanachama zaidi katika Kata hii.
Your Comment